WACHEZAJI sita wa klabu ya Shakhtar Donetski wamekataa kurejea nyumbani kufuatia mchezo wao wa kirafiki waliocheza nchini Ufaransa Jumamosi iliyopita kwasababu ya wasiwasi juu ya mgogoro wa Ukraine. Mji wa Donetski kwasasa unashikiliwa na waasi wanaotaka kujiunga na Urusi huku majeshi ya Ukraine wakitaka kuurejesha mji huo mikononi mwao. Wachezaji hao Alex Tixeira, Fred, Dentinho, Douglas Costa, Facundo Ferreyra na Ismaily hawakusafiri na wenzao baada ya mchezo huo wa kirafiki uliofanyika jijini Lyon. Rais wa klabu hiyo Rinat Akhmetov alionya kuwa wachezaji hao wanaweza kukumbwa na adhabu kama hawatarejea kutokana na mikataba yao waliyosaini. Hata hivyo Akhmetov amesema ana imani wachezaji hao wataheshimu mikataba yao na kurejea nyumbani kwa kipindi kifupi kijacho.
No comments:
Post a Comment