MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil, Neymar amedai kuwa walijitahidi kadri walivyoweza kuhakikisha wanalibakisha taji la dunia katika michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika hivi karibuni lakini walizidiwa uwezo na mataifa mengine hivyo inabidi wapambane wawafikie. Wakati akikataa kumlaumu kocha wa zamani wa Brazil Luiz Felipe Scolari, Neymar pia aliwaonya wachezaji chipukizi kuwa makini na baadhi ya makocha wanaoweza kuua vipaji vya chipukizi. Akiulizwa kuhusu kutolewa kwao katika michuano hiyo, Neymar amesema walilia kwasababu hiyo ilikuwa ni ndoto yao toka wakiwa wadogo kushinda taji hilo na walipambana kadri wanavyoweza kufikia walipofikia. Lakini nyota huyo amedai kuwa lazima wakiri kuwa kuna nchi sasa zimewapita kisoka na kujipanga kuona jinsi gani wanaweza kusifikia tena na kurejesha heshima yao. Neymar amesema anafikiri soka la Brazil liko nyuma, liko nyuma ya Ujerumani na Hispania kwa hiyo kama wameteleza na kurudi nyuma inatakiwa wajitutumue kiume na kukiri hilo ili waweze kusonga mbele.
No comments:
Post a Comment