MCHEZAJI WA STOKE AFELI VIPIMO VYA AFYA QATAR.
KIUNGO wa klabu ya Stoke City, Wilson Palacios ameshindwa kuchukuliwa na klabu ya Qatar Sports kufuatia kushindwa katika vipimo vya afya. Klabu hiyo ya Qatar ilibainisha Ijumaa kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Honduras aliwasili jijini Doha kwa ajili ya kumalisha hatua za mwisho za kuitumikia timu hiyo lakini bila kuweka wazi kilichomfanya kushidwa vipimo vya afya timu hiyo imethibitisha makubaliano hayo yamesitishwa. Klabu hiyo ilithibitisha taarifa hizo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa wameshindwa kuchukua kiungo huyo kutokana na kushindwa vipimo vya afya alivyoenda kufanyiwa. Palacios alijuunga na Stoke akitokea Tottenham Agosti mwaka 2011 lakini alishindwa kung’ara kutokana na kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 msimu uliopita alifanikiwa kucheza mechi 16 za Ligi Kuu pekee ingawa alikuwemo katika kikosi cha nchi yake kilichoshiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu.
No comments:
Post a Comment