KLABU ya Liverpool inakaribia kuzinasa saini za beki wa Southampton Dejan Lovren na mshambuliaji wa klabu ya Lille ya Ufaransa Divock Origi. Liverpool ambao kwasasa wako katika ziara yao nchini Marekani, wamekubalia kutoa paundi milioni 10 kwa ajili ya Origi mwenye umri wa miaka 19 ambaye anatarajiwa kusafiri kwa ajili ya vipimo vya afya siku chache sijazo. Mawingo ya Lovren mwenye umri wa miaka 25 yanatarajiwa kuanza upya pamoja na Southampton kukataa ofa ya kwanza ya Liverpool ya paundi milioni 20 wlaizotoa wiki zilizopita.
Nyota huyo wa kimataifa wa Croatia tayari ameshaonyesha nia yake ya kujiunga na Liverpool na klabu yake itabidi ilegeze msimamo wake. Lovren ambaye alijiunga na Southampton akitokea Lyon kwa ada ya paundi milioni 8.5 katika kipindi cha usajili wa majira kiangazi mwaka jana ameomba kuondoka baada ya kutumikia miezi 12 ya mkataba wake wa miaka minne.
No comments:
Post a Comment