KLABU kongwe ya Zamalek imetangaza kuwa imefikia makubaliano na kocha wa timu ya taifa ya Jordan Hossam Hassan kuingoza timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao. Zamalek ilimtimua Ahmed Hossam maarufu kama Mido juzi baada ya kupata sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe ya Congo, DRC. Maofisa wa klabu hiyo walitangaza kuwa na mazungumzo na Hossam Hassa ambaye alikubaliana na mambo yao na anatarajiwa kuingoza timu hiyo katika mchezo ujao dhidi ya AS Vita ya Congo, DRC itakayochezwa Agosti 10. Mkataba wa Hassan na timu ya taifa ya Jordan umemalizika toka Juni mwaka huu na pande zote hazijafikia makubaliano ya kuongeza mkataba mpya. Hassan ambaye aliwahi kuichezea Zamalek kati ya mwaka 2000 na 2004, pia aliwahi kuwa kocha wa timu hiyo kuanzia mwaka 2009 mpaka 2011.
No comments:
Post a Comment