KAMATI ya Ufundi ya Chama cha Soka cha Korea Kusini, imedai kuwa imepunguza orodha ya ya makocha wanaowania nafasi ya kuonoa timu ya taifa ya nchi hiyo na kubakiwa na makocha watatu wa kigeni. Kiongozi wa kamati hiyo Lee Yong-Soo aliwaambia waandishi wa habari kuwa kama ilikuwa na kazi ya kuchambua majina 17 ya makocha wazawa na 30 ya makocha wa kigeni mpaka kutoka orodha hiyo ya wlaiobakia. Aliyekuwa kocha wa nchi hiyo Hong Myung-Bo alijiuzulu wadhifa wake huo baada ya kampeni mbovu za michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil ambazo zilipelekea nchi kumaliza mkiani katika kundi lao wakiambulia alama moja. Yong-Soo majina matatu ya mwisho yaliyotoka ni ya makocha wa kigeni huku kocha mmoja pekee wa mzalendo akifikia viwango lakini baada ya majadiliano waliamua kumuondoa kwa kipindi hiki. Makocha waliopenya katika orodha hiyo ni pamoja na Neil Lennon aliyewahi kuinoa Celtic, nyota wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi Frank Rijkaard na kocha wa zamani wa Tottenham Hotspurs na Fulham Martin Jol.
No comments:
Post a Comment