MCHEZAJI nyota wa klabu ya Bayern Munich, Philipp Lahm ametangaza uamuzi wake wa kushtusha wa kustaafu soka la kimataifa baada ya Ujerumani kufanikiwa kunyakuwa Kombe la Dunia. Nahodha huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 30 aliliongoza taifa lake kuifunga Argentina kwa bao 1-0 katika mchezo wa fainali huku akicheza mechi saba katika michuano hiyo waliyoibuka na taji kwa mara ya kwanza toka waliponyakuwa taji la Ulaya mwaka 1996. Lahm alimuambia kocha wa timu hiyo Joachim Loew kuwa hataweza kupatikana tena kwa ajili ya kuichezea timu yake ya taifa. Nyota huyo amesema amefikiria kwa kina uamuzi wake huo na ameona huo ndio wakati muafaka kwake kustaafu na kuwaachia vijana wengine wadogo ili nao wapate nafasi hiyo adhimu. Lahm pia amesema amempigia rais Shirikisho la Soka la Ujerumani-DFB Wolfgang Niersbach kumpa taarifa hizo na kumshukuru yeye na watu wengine wote katika shirikisho hilo kwa ushirikiano waliompatia katika miaka hiyo michache. Lahm alichukua mikoba ya unahodha wan chi hiyo kutoka Michael Ballack mwaka 2011 ambapo mara ya kwanza kuvaa jezi ya Ujerumani ilikuwa katika mchezo dhidi ya Croatia ambao walishinda kwa mabao 2-1 Februari mwaka 2004.
No comments:
Post a Comment