Saturday, July 19, 2014

LAMPARD KUTIMKIA MAREKANI.

KIUNGO mkongwe wa zamani wa Uingereza, Frank Lampard anatarajia kumamilisha usajili katika klabu mpya ya Ligi Kuu ya Soka nchini Marekani-MLS ya New York City wiki ijayo. Klabu hiyo ilifanikiwa kumshawishi nyota huyo mwenye umri wa miaka 36 baada ya mkataba wake na Chelsea kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita. Kwasasa lampard yuko katika likizo fupi baada ya kuitumikia timu ya taifa ya Uingereza katika michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika nchini Brazil. Hata hivyo kiungo huyo anatarajiwa kujiunga na klabu hiyo mwanzoni mwa msimu mpya wa MLS mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment