Saturday, July 19, 2014

MOURINHO ADAI KUKAMILISHA USAJILI WA MAJIRA YA KIANGAZI.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amesema usajili wake katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi umekamilika kufuatia kumsajili beki wa kushoto Filipe Luis kutoka klabu ya Atletico Madrid. Luis anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Chelsea baada ya viungo Cesc Fabregas na Mario Pasalic pamoja na mshambuliaji Diego Costa. Akihojiwa Mourinho amesema wamemaliza usajili jana wakati muda rasmi wa kumalizika kwa usajili ni Agosti 31 na kuishukuru klabu yake kwa kazi nzuri sio kwasababu ya wachezaji walionunua bali kuweka rekodi kwa kusajili kwa muda mfupi. Chelsea wamekuwa wakihusishwa na tetesi za kuwataka wachezaji mbalimbali ghali katika kipindi hiki cha kiangazi akiwemo nyota wa Real Madrid na Ujerumani Sami Khedira na mshambuliaji wa Monaco radamel falcao. Hata hivyo Mourinho amesisitiza kuwa ameridhishwa na bishara waliyofanya klabu yake katika kipindi hiki kwani tayari wameshapata wachezaji wote waliowahitaji.

No comments:

Post a Comment