KLABU ya Liverpool imekubalia kumuuza mshambuliaji wake Fabio Borini kwenda klabu ya Sunderland kwa ada ya paundi milioni 14. Borini mwenye umri wa miaka 23 alikuwa akicheza kwa mkopo katika klabu hiyo msimu uliopita na kuisaidia isishuke daraja. Nyota huyo wa kimataifa wa Italia alifunga mabao 10 akiwa na Sunderland na kupelekea kuibuka na tuzo ya mchezaji bora wa mwaka anayechipukia. Borini ambaye alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha Brendan Rodgers wakati akitua Liverpool, alihamia Anfield akitokea Roma kwa ada ya paundi milioni 11 Julai mwaka 2012. Hata hivyo, mshambuliaji huyo kiwango chake kiliyumba toka alipotua Liverpool na kufunga mabao mawili katika msimu wa 2012-2013 kabla ya kupelekwa kwa mkopo Sunderland.
No comments:
Post a Comment