Saturday, July 19, 2014

SCHWEINSTEIGER APEWA NAFASI KUCHUKUA MIKOBA YA LAHM.

KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Ujerumani Bastian Schweinsteiger anapewa nafasi kubwa ya kuwa nahodha mpya wa mabingwa hao wa dunia baada ya Philipp Lahm kustaafu ghafla soka la kimataifa. Schweinsteiger alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Ujerumani wakati wakipambana kutafuta taji hilo la nne husani katika mchezo wa fainali dhidi ya Argentina pamoja na kuvuja damu nyingi kutokana na kupigwa kiwiko katika moja ya hekaheka ya fainali hiyo. Lahm alistaafu soka la kimataifa akiwa na umri wa miaka 30 baada ya kuichezea Ujerumani mechi 113. Pamoja na kwamba umri hauko pamoja na na Schweinsteiger kwani anatarajiwa kutimiza miaka 30 Agosti mosi mwaka huu wadau mbalimbali nchini humo wamekuwa wakimpa nafasi kutokana na uzoefu mkubwa alionao. Hata hivyo kocha wa Ujerumani Joachim Loew bado hajasema wakati atakaoamua kuteua nahodha mpya kwa nchi hiyo na hana haraka kutokana na mechi za kufuzu michuano ya Ulaya kutarajiwa kuanza Septemba.

No comments:

Post a Comment