KOCHA wa timu ya taifa ya Urusi Fabio Capello amesema anaweza kujiuzulu kama waajiri wake na wachezaji wa kikosi chake watapoteza imani naye. Akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza toka Urusi ishindwe kuvuka hatua ya makundi katika michuano ya Kombe la Dunia, kocha huyo wa zamani wa Uingereza amesema anategemea sana kuungwa mkono na kuaminiwa kwa kile anachokifanya. Kocha liendelea kudai kuwa huwa anafanya kazi kwa kuangalia na shauku kama akiona anaungwa na wote wanaomzunguka na kama akiona imani hiyo imetoweka atajiuzulu mwenyewe. Capello aliongeza mkataba wake wenye thamani ya euro milioni tisa kwa mwaka Januari mwaka huu ambapo utamalizika baada ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 itakayofanyika nchini humo. Naye rais wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo, Nikolav Tolstykh aliondoa shaka kwamba hakuna yeyote mwenye mpango wa kumtimua kocha huyo kwasasa ambapo hakuna mjumbe yeyote wa kamati ya utendaji anayetaka Capello aondoke.
No comments:
Post a Comment