LIGI Kuu nchini Uingereza imetangaza jana kuwa waamuzi watakaochezesha mechi za ligi hiyo watatumia dawa maalumu ya kupuliza kwa ajili ya kutambua eneo la mipira ya adhabu katika msimu wa mwaka 2014-2015. Katika taarifa yake iliyotumwa katika mtandao wa kijamii wa twitter ilithibitisha kufanyika kwa suala hilo kama ilivyokuwa ikifanyika katika michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika nchini Brazil. Dawa hiyo maalumu iliyo katika mfumo wa povu ambayo huyayuka ndani ya dakika moja, hupuliziwa katika uwanja na mwamuzi kutambua eneo ambalo mpira wa adhabu utapigwa na umbali ambapo wachezaji wanatakiwa kuweka ukuta kwa ajili ya kuzuia adhabu hiyo. Dawa hiyo ya kupuliza imeonekana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katika Kombe la Dunia mpaka kupelekea kukubalika na Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA ambapo nao wataitumia katika mechi za Ligi ya Mabingwa na Europa League. Utaratibu huo pia aunatarajiwa kutumika katika msimu mpya wa Ligi Kuu nchini Ufaransa.
No comments:
Post a Comment