RAIS mkongwe wa Chama cha Soka nchini Argentina-AFA na makamu wa rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Julio Grondona amefariki dunia jan akiwa na umri wa miaka 82 katika kliniki moja huko Buenos Aires. Kiongozi huyo mkongwe ambaye amekuwa rais wa AFA kuanzia mwaka 1979 alipelekwa hospitali akisumbuliwa na matatizo ya moyo na alifariki wakati akifanyiwa upasuaji wa dharura. Mapema wiki hii rais huyo alifanya mazungumzo na Alejandro Sabella ambaye aliamua kutoendelea kuwa kocha wa Argentina baada ya kuingoza timu hiyo kutinga fainali ya michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika nchini hivi karibuni. Grondona amekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA toka mwaka 1988 akiongoza kamati ya fedha na alichaguliwa kuongoza AFA miaka tisa kabla na serikali ya kijeshi iliyokuwa madarakani. Amekuwa akichaguliwa kwa mafanikio kuendelea kuwa kiongozi wa AFA kila baada ya miaka minne toka mwaka 1979 huku akiungwa mkono vilabu zaidi ya 22,000 vya nchi hiyo. Akiwa madarakani kwa kipindi chote hicho Grondona amefanikiwa kuiwezesha nchi hiyo kushinda taji la Kombe la Dunia mwaka 1986 nchini Mexico, Copa Amerika mwaka 1991 na 1993 na kupata medali ya dhahabu katika michuano ya olimpiki mwaka 2004 na 2005.
No comments:
Post a Comment