MSHAMBULIAJI mpya aliyesajiliwa na Arsenal, Alexis Sanchez anatarajiwa kuripoti kambini tayari kwa mazoezi lakini kuna uwezekano akaikosa ziara ya siku nne ya mazoezi ya timu hiyo huko Austria. Sancehz aliyesajili kwa paundi milioni 30 ameanza maisha rasmi kama mchezaji wa Arsenal leo kufuatia uhamisho wake kutokea Barcelona lakini anatakiwa kuhakiki kibali chake cha kusafiria jijini Paris kabla ya kutua London. Arsenal walirejea kutoka katika ziara yao ya siku nne nchini Marekani jana ambapo walichapwa bao 1-0 na New York Red Bulls na wanatarajiwa kufanya mazoezi leo asubuhi kabla ya kusafiri kwenda Austria. Sanchez ambaye atabakia nchini Uingereza akifanya kazi na makocha wa viungo anaweza kucheza mechi yake ya kwanza katika michuano ya Kombe la Emirates dhidi ya Benfica Jumamosi hii. Wachezaji wenzake waliosajiliwa msimu huu beki wa kimataifa wa Ufaransa, Mathieu Debuchy, golikipa wa Colombia David Ospina na bekiwa Southampton Calum Chambers nao wanatajiwa kuripoti kambini wiki hii.
No comments:
Post a Comment