BEKI wa kimataifa wa Ufaransa, Eric abidal ambaye alifanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini mwaka 2012, naye ametangaza kustaafu soka la kimataifa. Abidal mwenye umri wa miaka 34 ambaye ameichezea nchi yake mechi 67, anafuata nyayo za Franck Ribery na kiungo wa Manchester City Samir Nasri kufunga pazia lao la michuano ya kimataifa. Abidal ambaye kwasasa anachezea Olympiakos ya Ugiriki baada ya kuzichezea pia Barcelona na Monaco amedai kuchukizwa na hatua ya kutoitwa katika kikosi cha nchi hiyo kilichokwenda kwenye Kombe la Dunia nchini Brazil. Beki huyo ambaye aliitumikia Barcelona kwa miaka sita kuanzia mwaka 2007, aligundulika kuwa uvimbe katika ini Machi mwaka 2011 na mwaka mmoja baadae alifanyiwa upasuaji wa kupandikiza lingine. Alijiunga na Monaco Julai mwaka jana baada ya Barcelona kuamua kutomuongeza mkataba mwingine.
No comments:
Post a Comment