Thursday, August 14, 2014

TANZANIA YARUDI NYUMA TENA VIWNAGO FIFA.

TANZANIA imeporomoka tena kwa nafasi nne katika viwango vya ubora duniani vinavyoandaliwa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA na kutolewa kila baada ya mwezi mmoja. Katika viwango vilivyotolewa mwezi uliopita Tanzania walipanda mpaka kufikia nafasi ya 106 lakini kwa mwezi huu wameporomoka mpaka nafasi ya 110 wakizidiwa na majirani zao wa Afrika Mashariki Uganda waliopo katika nafasi ya 81 na Kenya waliopo nafasi ya 104. Kwa upande wa Afrika Algeria bado wanaendelea kuongoza kwa kuwa nafasi ya 24 wakifuatia Ivory Coast waliopo nafasi ya 25, Nigeria wanashikilia nafasi ya tatu huku nafasi ya nne na tano zikishikiliwa na Ghana na Misri waliopo nafasi ya 36 na 38. Mabingwa wa dunia Ujerumani wao ndio vinara katika viwango hivyo huku kukiwa hakuna mabadiliko katika nafasi zinazofuata kulinganisha na mwezi uliopita ambapo Argentina wapo nafasi ya pili wakifuatiwa na Uholanzi, Colombia, Ubelgiji na Uruguay. Mabingwa wa zamani wa dunia Hispania wao wamepanda katika nafasi moja na sasa wamefungana na Brazil katika nafasi ya saba huku nafasi ya nafasi ya nane ikishindwa na Uswis, Ufaransa wako nafasi ya tisa na kumi bora inafungwa na Ureno.

No comments:

Post a Comment