Thursday, August 14, 2014

MOURINHO AMFUNGULIA MILANGO MOSES.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amedokeza uwezekano wa kuuzwa kwa winga Victor Moses mwishoni mwa dirisha la usajili kiangazi hiki. Moses alijiunga na Chelsea mwaka 2012 kwa ada ya paundi milioni tisa akitokea Wigan Athletic lakini amekuwa akipata wakati mgumu kupata nafasi katika kikosi cha kwanza toka alipotua Stamford Bridge. Hatua hiyo ilipelekea nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 kupelekwa kwa mkopo Liverpool msimu uliopita na sasa anaweza kuondoka kuondoka moja kwa moja. Mourinho amesema Moses kwasasa anacheza katika nafasi ambayo wapo wachezaji wengi wanaoimudu vyema hivyo kuna uwezekano akamuuza kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili kiangazi hiki. Moses amefunga bao moja pekee la ligi katika mechi 23 ambazo ameichezea Chelsea.

No comments:

Post a Comment