KOCHA Stephen Keshi amekataa mkataba mpya aliopewa na Shirikisho la Soka nchini Nigeria-NFF kwa ajili ya kuendelea na kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo. Hivi karibuni mjumbe mmoja wa NFF alidai kuwa pande zote mbili yaani Keshi na shirikisho hilo tayari walishafikia makubaliano ya mkataba mpya na kilichobakia na kusaini. Mkataba huo sasa umekataliwa na Keshi ambaye anataka zaidi ya dola 62,000 zilizotolewa na NFF kama mshahara wake kwa mwezi. Keshi alikuwa akilipwa kiasi cha dola 31,000 kabla ya mkataba wake haujamalizika baada ya michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Brazil mwaka huu. Pamoja na kuongezwa mshahara huo kwa asilimia 100, Keshi bado hajashawishika kama hicho ni kiwango sahihi anachostahili kama akiendelea kuinoa timu hiyo. Keshi amesema kiwango chake cha ufundishaji ni kikubwa kuliko dola 31,000 au 62,000 kwani kuba klabu moja nchini Angola iko tayari kumlipa mpaka dola 111,000.
No comments:
Post a Comment