MENEJA wa klabu ya Bayern Munich, Pep Guardiola amedai kuwa anahitaji muda zaidi wa kujindaa kwa ajili ya msimu wa Ligi Kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga. Bayern walianza kampeni zao msimu wa 2014-2015 kwa mchezo wa Super Cup dhidi ya mahasimu wao Borussia Dortmund, mchezo ambao walitandikwa mabao 2-0 na kikosi hicho kinachonolewa na Jargen Klopp. Dortmund ambao walimaliza katika nafasi ya pili katika Bundesliga na Kombe la Ligi msimu uliopita walifanikiwa kutetea taji lao hilo ambalo pia walilichukua mwaka jana. Guardiola amesema katika mchezo huo walicheza vizuri katika dakika 15 za kwanza lakini baadae wakaanza kufanya makosa mengi ambayo yaliwagharimu. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa bado wanahitaji muda wa kujiandaa kwani walijaribu kucheza vizuri lakini walipata tabu kumiliki mchezo.
No comments:
Post a Comment