Thursday, August 14, 2014

SPURS YANASA BEKI LA KIMAREKANI.

KLABU ya Tottenham Hotspurs imefanikiwa kumsajili beki wa kimataifa wa Marekani DeAndre Yeldin kutoka klabu ya Seattle Sounders. Yeldin mwenye umri wa miaka 21 amesaini mkataba wa miaka minne na Spurs lakini anataendelea kubakia Sounders kabla ya kutua London mwanzoni mwa msimu wa 2015-2016. Beki huyo ameichezea timu ya taifa ya Marekani mechi saba na alikuwemo katika kikosi cha nchi hiyo kilichotinga hatua ya timu 16 bora katika Kombe la Dunia nchini Brazil chini ya kocha Jurgen Klinsmann ambaye aliwahi kuwa mshambuliaji wa Spurs. Akihojiwa Yeldini amesema ana hamu kubwa ya kucheza katika Ligi Kuu na kujipa changamoto mwenyewe dhidi ya baadhi ya wachezaji bora kabisa duniani. Yeldini aliendelea kudai kuwa alifanya mazungumzo na Klinsmann na ameunga mkono kwa kiasi kikubwa mpango huo nay eye ndio sababu ya uamuzi wake huo.

No comments:

Post a Comment