BEKI wa kimataifa wa Ivory Coast, Kolo Toure amekataa uhamisho wa kwenda Trabzonspor lakini amesema chochote kinaweza kutokea baada ya kuapa kubakia Liverpool kwa kipindi hiki. Toure alionekana kama ataondoka Anfield baada ya rais wa klabu hiyo ya Uturuki Ibrahim Haciosmanoglu kudai kuwa tayari walishafikia makubaliano na mchezaji huyo wa zamani wa vilabu vya Manchester City na Arsenal. Akihojiwa Toure alikiri kuwa klabu hiyo ilikuwa ikimhitaji lakini anafurahi kuwa mchezaji wa Liverpool hususani baada ya kocha wake Brandan Rodgers kuonyesha imani naye na kumuingiza katika mipango yake. Toure amesema Rodgers anamhitaji ili aweze kuisaidia timu hiyo kushindana katika mshindano yote waliyokuwemo kutokana na uzoefu aliokuwa nao.
No comments:
Post a Comment