KLABU ya Bayern Munich imetangaza kufikia makubaliano na Real Madrid juu ya uhamisho wa Xabi Alonso kwa ada ambayo haikuwekwa wazi huku nyota huyo wa kimataifa wa Hispania akisafiri leo kwenda Ujerumani kwa ajili vipimo vya afya. Mabingwa hao wa Bundesliga wamepania kuimarisha safu yao ya kiungo kwa kuongeza kiungo katika kikosi chao kutokana na majeruhi yaliyowaandama wachezaji wake kama Javi Martinez, Bastian Scheinsteiger na Thiago Alcantara. Mjumbe wa bodi wa Bayern Jan-Christian Dreesen alithibitisha kuwa ni kweli wamefanya mazungumzo na Madrid pamoja na Alonso na tayari wameshafikia makubaliano kilichoabaki ni vipimo vya afya. Alonso alisaini mkataba mpya na Madrid unaomalizika mwaka 2016 mwapema mwaka huu lakini amepoteza namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo huku kocha Carlo Ancelotti akipendelea kuwatumia zaidi viungo Luka Modric, Tony Kroos na James Rodriguez. Kiungo huyo ambaye ametangaza kustaafu soka la kimataifa wiki hiialianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Real Sociedad na pia amewahi kuzicheza Eibar na Liverpool kabla ya kujiunga na Madrid katika majira ya kiangazi mwaka 2009.
No comments:
Post a Comment