BAADA ya sare ya bila kufungana dhidi ya mahasimu wao AS Vita katika mchezo wa jana uliochezwa jijini Kinsasha, TP Mazembe wamekwenda katika nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika huku wakiwa vinara wa kundi A. Katika mchezo wa jana Vita walicheza bila ya mshambuliaji wao Dady Birori ambaye alisimamishwa na Shirikisho la Soka la Afrika-CAF kwa kutumia majina mawili tofauti katika klabu yake na timu ya taifa ya Rwanda. Sakata hilo la Birori limepelekea Rwanda kuondolewa katika makundi ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwakani. Timu zote hizo mbili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimemaliza katika zikiwa na alama 11 ila Mazembe wameongoza kundi hilo kwa kuwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa. Sasa Mazembe watacheza mchezo wao wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ugenini dhidi ya ES Seif ya Algeria huku Vita wao wakiwakaribisha CS Sfaxien ya Tunisia ambapo mechi za mkondo wa kwanza zikitarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 19, 20 au 21.
First leg: September 19-21, second: September 26-28.
First leg: September 19-21, second: September 26-28.
No comments:
Post a Comment