RAIS wa klabu ya Barcelona, Josep Maria Bartomeu amekiri kufanyika makosa katika usajili wa wachezaji walio chini ya umri lakini wanatarajia kukata rufani Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS kupinga adhabu ya kufungiwa kusajili misimu miwili. Shirikisho la Soka Duniani-FIFA lilitupilia mbali rufani ya Barcelona waliyowapa kwa kosa hilo hivyo kumaanisha kuwa hawataruhusiwa kusajili kuanzia dirisha dogo la usajili Januari na Julai hadi Agosti mwakani. Adhabu hiyo ilisimamishwa kwa muda kupisha kusikilizwa kwa rufani yao hivyo kuwapa nafasi ya kusajili katika kipindi hi9ki cha kiangazi ambapo wamefanikiwa kumnasa Luis Suarez lakini Bartomeu amesema sasa wanatarajia kupeleka rufani yao CAS ili wapunguziwe adhabu. Bartomeu amesema wanajua kuwa walifanya makosa lakini adhabu imekuwa kubwa sana hivyo wataandaa ushahidi mzuri ili wa kuupeleka CAS ili wapunguziwe adhabu hiyo.
No comments:
Post a Comment