KLABU ya Manchester United imekubali kutoa kitita kilichovunja rekodi ya usajili nchini Uingereza cha paundi milioni 59.7 kwa ajili ya kumsajili winga wa Real Madrid Angel Di Maria. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 26 tayari ameshatua jijini Manchester na ameshafanyiwa vipimo vya afya asubuhi ya leo na baadae atatambulishwa rasmi. Di Maria anaweza kucheza mechi yake ya kwanza ugenini wakati United watakapocheza na Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu Jumamosi hii.
Usajili huo unazidi paundi milioni 50 walizolipa Chelsea kwa ajili ya kumchukua Fernando Torres kutoka Liverpool mwaka 2011. Mara ya mwisho United kuvunja rekodi ya usajili nchini Uingereza ilikuwa mwaka 2002 wakati walipotoa kitita cha paundi milioni 29.1 kwa ajili beki Rio Ferdinand alitoa Leeds United. Mpaka sasa United wameshatumia kiasi cha paundi milioni 132 kwa ajili ya usajili wa majira ya kiangazi wakiwa tayari wameshawasajili beki Luke Shaw, kiungo Ander Herrera na Marcos Rojo.
No comments:
Post a Comment