MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Diego Simeone amefungiwa mechi nane na Shirikisho la Soka nchini Hispania-RFEF jana kufuatia kuitolewa na hatua za hasira alizochukua wakati wa mchezo wa Super Cup dhidi ya Real Madrid. Kocha huyo raia wa Argentina alifungiwa mechi nne kwa kosa la kumtandika kofi mwamuzi wa nne nyuma ya kichwa baada ya kuondolewa katika benchi lake ufundi Ijumaa iliyopita, adhabu ya mechi mbili ikiwa ni kwasababu ya kulalamika, moja ya kupinga uamuzi na nyingine kwa kutoa maelekezo katika benchi lake la ufundi akiwa jukwaani. Katika taarifa yake RFEF imedai kuwa Simeone alitolewa kwa kosa la kulalamika huku akinyoosha mikono yake hewani na kutoka nje ya eneo lake zaidi ya mara moja na kugoma kusikilisha maelezo ya mwamuzi wa nne. Tukio hilo lilitokea katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo dhidi ya Madrid katika Uwanja wa Calderon ambao Atletico walishinda kwa bao 1-0 hivyo kuwafanya kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2-1 katika mechi wlaizokutana. Baadae Simeone alikiri kuwa alifanya makosa lakini Atletico wanatarajia kukata rufani ili adhabu hiyo iweze kupunguzwa kidogo.
No comments:
Post a Comment