MSHAMBULIAJI mkongwe wa Ivory Coast, Didier Drogba ametangaza kustaafu soka la kimataifa akiwa na umri wa miaka 36. Mshambuliaji huyo wa Chelsea aliiwakilisha nchi yake katika michuano ya Kombe la Dunia kiangazi hiki nchini Brazil lakini sasa ameamua kuhamishia nguvu zake katika klabu baada ya kufunga mabao 65 katika mechi 104 akiwa na Ivory Coast. Katika taarifa yake Drogba amedai kuwa limekuwa ni jambo la kusikitisha sana kuamua kustaafi soka la kimataifa kwa katika miaka 12 aliyotumikia nchi yake imekuwa na msisimko mkubwa. Drogba amesema toka alipoitwa kwa mara ya kwanza mpaka mechi yake ya mwisho amekuwa akijitoa kwa hali na mali kuisaidia nchi yake. Pia amedai anajivunia kuwa nahodha wa Ivory Coast kwa miaka nane na mchango alioutoa katika kipindi chote hicho ambacho amekuwa sehemu ya kikosi chake.
No comments:
Post a Comment