MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Colombia, James Rodriguez amepokea tuzo yake ya Kiatu cha Dhahabu katika sherehe maalumu zilizofanyika jijini Madrid. Nyota huyo anayekipiga Real Madrid alifunga mabao sita wakati wa michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil akiwazidi nyota wengine kama kama Thomas Muller aliyefunga mabao matano, neymar, Lionel Messi na Robin van Persie ambao walifunga mabao manne. Rodriguez mwenye umri wa miaka 23 alifunga bao moja katika mchezo dhidi ya Ugiriki, Ivory Coast, Japan na Brazil wakati akifunga mabao mawili katika mchezo wa mtoano dhidi ya Uruguay. Akipokea tuzo hiyo, Rodriguez amesema anajivunia kwasababu ilikuwa ni ndoto zake, anamatumaini ya kushinda zaidi na anadhani yuko katika klabu sahihi katika kufikia malengo hayo.
No comments:
Post a Comment