MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Uruguay, Luis Suarez ameondoka katika Mahakama ya Michezo ya Kimataifa kufuatia kusikilizwa kwa rufani yake ya kufungiwa miezi minne ambayo inatatarajiwa kutolewa baadae. Nyota huyo wa Barcelona amefungiwa kujishughulisha na mambo ya soka huku akifungiwa mechi tisa za kimataifa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kufuatia kumng’ata Giorgio Chiellini wakati wa ushindi wa Uruguay wa bao 1-0 katika kundi D dhidi ya Italia katika Kombe la Dunia June 26 mwaka huu. Lakini nyota huyo wa zamani wa Liverpool amemua kupinga uamuzi huo na timu yake ya mawakili imedai kuwa wana anafasi kubwa ya kupunguza adhabu aliyopewa mchezaji huyo. Uamuzi kuhusu adhabu hiyo ya Suarez kama itapunguzwa utajulikana leo lakini utatangazwa hadharani wiki ijayo. Suarez alilimwa adhabu hiyo kubwa na kali na FIFA kutoka na tukio hilo la Chiellini ambalo limekuwa ni la tatu sasa.
No comments:
Post a Comment