KLABU ya Manchester United italazimika kuvunja rekodi ya usajili nchini Uingereza kwa ajili ya kumsajili winga mahiri wa klabu ya Real Madrid Angel Di Maria. Meneja wa Madrid Carlo Ancelotti amebainisha kuwa Di Maria mwenye umri wa miaka 26 tayari amekwishawaaga wachezaji wenzake kuelekea katika uhamisho wake huo. Inakadiriwa kuwa United italazimika kuilipa Madrid kitita cha paundi milioni 75 kama wanahitaji saini ya winga huyo. Kama kweli wakitoa kitita hicho watakuwa wamevunja rekodi ya usajili iliyowekwa na Chelsea wakati walipomsajili Fernando Torres kwa paundi milioni 50 kutoka Liverpool mwaka 2011. Usajili mkubwa uliowahi kuweka rekodi na kufanywa na United ulikuwa ni wa Rio Ferdinand ambaye alitua Old Trafford kwa paundi milioni 29.1 akitokea Leeds mwaka 2002. Di Maria alitua Madrid akitokea Benfica kwa ada ya paundi milioni 36 mwaka 2010 na kufanikiwa kushinda taji la La Liga mwaka 2012 na Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment