MENEJA wa zamani wa klabu ya Barcelona, Gerardo Martino ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Argentina akichukua nafasi ya Alejandro Sabella. Martino mwenye umri wa miaka 51 aliondoka Barcelona mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuinoa timu hiyo kwa mwaka mmoja na kushinda taji lolote kubwa kwa mara ya kwanza toka msimu wa 2007-2008. Kocha huyo amewahi kuifundisha Paraguay kati ya mwaka 2006 na 2011 na kuwapaisha mpaka katika robo fainali katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 iliyofanyika Afrika Kusini. Sabella aliikacha Argentina baada ya kufungwa bao 1-0 na Ujerumani katika fainali ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu. Martino alichukua nafasi ya Tito Vilanova Barcelona Julai mwaka 2013 na kusaini mkataba wa miaka miwili na timu hiyo.
No comments:
Post a Comment