MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amehoji mpango uliotumika kumruhusu kiungo wa zamani wa Chelsea Frank Lampard kujiunga na Manchester City kwa mkopo kutoka timu ya New York City FC ambayo inamilikiwa na City. Mbali na Lampard kwenda Etihad Stadium, New York pia imempeleka kwa mkopo mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania David Villa katika timu ya Melbourne City ya Australia ambapo vilabu vyote vitatu vinamilikiwa na City. Wenger ambaye kikosi chake kitakwaana na City mwishoni mwa wiki hii katika mchezo wa Ngao ya Hisani anadhani kuwa mahusiano baina ya vilabu hivyo inaweza kuipa uwiano usiofaa mabingwa hao wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Kauli hiyo Wenger imekuja baada ya kuhojiwa kuhusiana na uhamisho wa Lampard, ambapo amesema ameshangazwa lakini inavyoonekana vilabu hivyo vitakuwa vikiilisha Man City kwani amesikia kuwa wana mpango wa kununua vilabu vitano kutoka sehemu mbalimbali duniani. Wenger amesema hafahamu vyema sheria zilivyo kwani kwasasa wachezaji wanaowasajili hawawezi kucheza mpaka mwakani hivyo wanawachukua halafu wanawapeleka kwa mkopo.
No comments:
Post a Comment