KLABU ya Arsenal inasubiri matokeo ya ya vipimo vya kifundo cha mguu cha Olivier Giroud baada ya wasiwasi kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa anaweza kukaa nje kwa miezi mitatu. Giroud mwenye umri wa miaka 27 alipata majeruhi hayo katika mchezo dhidi ya Everton uliomalizika kwa sare vya mabao 2-2. Nyota huyo anatakiwa kufanyiwa vipimo kwa mara nyingine ili kujua ukubwa wa tatizo na muda ambao linaweza kupona. Kukosekana kwa Giroud kunamuacha meneja wa Arsenal Arsene Wenger kubakiwa na Alexis Sanchez, Joel Campbell, Yaya Sanogo na Lukas Podolski kama machaguo yake katika safu ya usambuliaji. Sanogo naye alikuwa nje kutokana na matatizo ya msuli na kuna hati hati akaukosa mchezo wa kesho wa kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Besiktas huku Sanchez yeye amekuwa akitumika kama winga toka atue akitokea Barcelona msimu huu.
No comments:
Post a Comment