MENEJA wa klabu ya Real Madrid, carlo Ancelotti ameifananisha timu hiyo na injini ya diesel huku akiwa na uhakika kuwa kikosi chake kitasahau kuanza kwa kusuasua wakati wakijiandaa na mchezo dhidi ya Atletico Madrid Jumamosi hii. Timu hizo mbili ambazo zinatoka mji mmoja, zimejijengea uhasama hususani baada ya kutua kocha Diego Simeone kutua Atletico na kuifanya timu hiyo kuwa ya ushindaji wa mataji. Ingawa bado mapema sana toka kuanza kwa la Liga, Madrid wanahitaji kuzinduka baada ya kukubalia kipigo kutoka kwa Real Sociedad katika mchezo wao wa pili. Akihojiwa Ancelotti amesema anajua timu yake imeanza kwa kusuasua kama injini ya diesel lakini kutokana na bidii waliyoonyesha mazoezini ana uhakika watakuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo wa Jumamosi. Kocha aliendelea kudai kuwa pamoja na kuwakosa nyota wake Angel Di Maria aliyekwenda Manchester United na Xabi Alonso aliyekwenda Bayern Munich huku Sami Khedira akiwa majeruhi, bado ana imani kubwa ya kufanya vizuri.
No comments:
Post a Comment