Thursday, September 11, 2014

KUFA KUFAANA: MAJERUHI YA REUS YAMPA NAFASI KAGAWA DORTMUND.

MENEJA wa klabu ya Borussia Dortmund Jurgen Klopp anatumaini Shinji Kagawa anaweza kuacha kucheza moja kwa moja kufuiatia matatizo ya majeruhi ya Marco Reus. Mara ya kwanza Klopp alitegemea kuanza taratibu na Kagawa baada ya kupitia kipindi kigumu katika miaka miwili aliyoichezea Manchester United. Lakini kutokana na majruhi ya Reus, Klopp amesema hana jinsi bali kumgeukia kiungo huyo wa kimataifa wa Japan ili aweze kuziba nafasi hiyo. Klopp ameendelea kudai kuwa anajua kwamba Kagawa hawezi kuwa fiti kama alivyoondoka katika klabu hiyo mara ya kwanza lakini anadhani amzingira ya hapo anayajua hivyo hayatampa tabu. Kabla ya kuondoka kwenda United, Kagawa aliifungiwa Dortmund mabao 21 katika mechi 49 alizoichezea timu hiyo.

No comments:

Post a Comment