MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers amesema kuwa majeruhi ya Daniel Sturridge yangeweza kuepukika na Chama cha Soka cha Uingereza kinapaswa kuwaepusha wachezaji na majeruhi pindi wawapo katika majukumu ya kimataifa. Mshambuliaji huyo alicheza kwa dakika 89 wakati Uingereza ikishinda bao 1-0 dhidi ya Norway katika Uwanja wa Wembley Jumatano iliyopita kabla ya kurejea tena mazoezini saa 36 baadae na kupata majeruhi akiwa mazoezini. Sturridge mwenye umri wa miaka 25 alikosa mchezo ambao Uingereza iliibugiza mabao 2-0 Swtzerland katrika mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya Jumatatu kutokana na majeruhi hayo na sasa anatarajiwa kukaa nje kwa wiki mbili zaidi. Rodgers amesema wamesikitishwa sana kutokana kazi kubwa aliyofanya wakati wa maandalizi ya msimu kwani wanadhani majeruhi aliyopata yalikuwa yanaepukika kama wahusika wangekuwa makini. Liverpool itajitupa uwanjani Jumamosi hii kukwaana na Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu.
No comments:
Post a Comment