Thursday, September 11, 2014

MESSI BADO ANA ANAFASI YA KUSHINDA KOMBE LA DUNIA - PELE.

NGULI wa soka wa Brazil Pele amesisitiza kuwa Lionel Messi bado ana nafasi ya kushinda taji la Kombe la Dunia na kuongeza kuwa nyopta huyo wa Barcelona bado ni mchezaji bora hata kama ameshindwa kuingoza Argentina kushinda taji hilo. Messi mwenye umri wa miaka 27 alikaribia kubeba taji la Kombe la Dunia kiangazi hiki lakini Ujerumani waliwazidi maarifa na kuonyesha kwamba wao ndio katika mchezo wa fainali waliokutana. Hata hivyo Pele ameweka wazi kuwa maisha ya soka kwa Messi bado hayajaisha na anaamini anaweza kupata nafasi nyingine tena katika michuano ya kombe la Dunia itakayofanyika nchini urusi mwaka 2018. Pele amesema Messi ni mchezaji aliyekamilika na ana umbo zuri hivyo hana ashaka kwamba atakuwepo katika michuano ya Kombe la dunia inayokuja. Messi ameichezea Argentina mechi 93 mpaka sasa na kufunga mabao 42.

No comments:

Post a Comment