Thursday, September 11, 2014

PISTORIUS AKWEPA KITANZI.

JAJI anayetoa uamuzi katika kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius, amesema upande wa mashitaka umekosa kuthibitishia kikamilifu shitaka kuu la kwanza dhidi ya Pistorius kuwa alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp. Hata hivyo jaji huyo Thokozile Masipa amepinga ushahidi wa upande wa utetezi kwamba mwanariadha huyo hakunuia kutenda uhalifu alipomuua mpenzi wake Reeva. Pistorius alikiri kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwaka jana lakini amekana kumuua kwa maksudi , akisema alidhani kuwa mwizi alikuwa amevamia nyumba yake. Upande wa mshitaka unasisitiza kuwa Pistorius alimuua Steenkamp kwa maksudi ,baada ya wapenzi hao wawili kutofautiana. Kwa mujibu wa BBC, Jaji huyo anaweza kuchukua hadi Ijumaa mpaka kumaliza kutoa uamuzi wake kuhusiana na kesi hiyo.

No comments:

Post a Comment