WINGA mahiri wa klabu ya Bayern Munich, Franck Ribery anatarajiwa kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wake wa msimu huu wakati timu yake itakapokwaana na VfB Stuttgart Jumamosi.Ribery amekuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua lakini sasa anaonekana kuwa fiti. Bayern ambao ni mabingwa watetezi wa Bundesliga wameanza kwa kusuasua msimu huu kuliko ilivyokuwa kwa msimu uliopita kufuatia sare ya bao 1-1 dhidi ya Schalke katika mchezo wao wa pili. Kwasasa wasiwasi upo kwa kiungo mpya aliyesajiliwa kiangazi hiki Xabi Alonso ambaye alikosa mazoezi wiki hii kutokana na kuumia mguu na ndio kwanza maenaza kukimbia tena. Winga mahiri wa kimataifa wa Uholanzi, Arjen Robben naye pia amefanya mazoezi peke yake kutokana na majeruhi ya kifundo cha mguu wakati beki Rafinha naye akiwa bado nje kutokana na majeruhi ya goti. Kurejea kwa ribery ambaye mapema mwezi huu alitangaza kustaafu soka la kimataifa kunakuwa ahueni kubwa kwa Bayern kuelekea katika mchezo wao huo muhimu wa Jumamosi.
No comments:
Post a Comment