Monday, September 22, 2014

BILIONEA LA SINGAPORE LANUNUA HISA KATIKA TIMU YA KINA GIGGS.

BILIONEA Peter Lim ambaye aliwahi kujaribu kuinunua Liverpool na akikaribia kuichukua Valencia, amenunua hisa za asilimia 50 za timu ya daraja la kwanza kanda ya kaskazini ya Salford City. Nyota wa zamani wa Manchester United Gary na Phil Neville, Ryan Giggs, Paul Scholes na Nicky Butt ambao walikubali kuinunua klabu hiyo Machi mwaka huu nao watamiliki hisa asimilia 50. Katika taarifa yao nyota hao wamedai kuwa uzoefu alionao Lim katika biashara hizo utawasaidia kwa kiasi kikubwa sana. Bilionea huyo raia wa Singapore mwenye umri wa miaka 61 anakadiriwa na jarida la Forbes kuwa na utajiri unaofikia kiasi cha paundi bilioni 1.5 lakini aliondoa zabuni ya paundi milioni 320 ili ainunue Liverpool mwaka 2010. Nyota hayo wamedai kuwa wamefahamiana na Lim kwa zaidi ya miaka 10 na wanategemea mambo ya kusisimua kwa Salford ambao wanaongoza ligi yao ambayo kwa Uingereza ni Ligi Daraja la Nane.

No comments:

Post a Comment