Monday, September 22, 2014

KOMBE LA DUNIA 2022 HALITAFANYIKA QATAR - ZWANZIGER.

MJUMBE wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Theo Zwanziger amesema michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 haitaweza kufanyika Qatar kutokana na joto kali katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati. Zwanziger ambaye ni raia wa Ujerumani aliliambia jarida la michezo la Bild jana kuwa anadhani mwisho wa siku michuano ya Kombe la Dunia 2022 haitafanyika katika nchi hiyo. Mjumbe huypo aliendelea kudai kuwa watabibu wamesema hawatakubalia kuwajibika kama michuano hiyo itafanyika katika hali ya hatari kama hiyo. Ingawa Qatar wamesisitiza ambao ni matajiri wakubwa wa mafuta wamesisitiza kuwa wanaweza kuandaa michuano hiyo majira ya kiangazi kwa kutumia teknologia ya vipoza hewa katika viwanja vyake, sehemu za mazoezi na mahali watakapofikia mashabiki bado kumekuwa na wasiwasi mkubwa kuhusiana na afya za wachezaji na mashabiki watakaokuja kushuhudia michuano hiyo. Zwanziger amesema anajua wanaweza kuweka vipoza hewa viwanjani lakini Kombe la Dunia halichezwi viwanjani pekee kwani mashabiki kutoka duniani kote watakwenda na kusafiri katika hali hiyo ya joto jambo ambalo ni hatari kwa afya na maisha yao. Michuano ya mwaka 2022 imekuwa ikileta mjadala mkubwa huku rais wa FIFA Sepp Blatter akikiri kuwa walifanya makosa kuipa Qatar kuandaa michuano hiyo na kutaka kuangalia uwezekano wa kuamisha michuano hiyo ichezwe katika majira ya baridi.

No comments:

Post a Comment