KLABU ya JS Kabylie imefungiwa kushiriki katika michuano ya Afrika kwa miaka miwili kufuatia shambulio lililosababisha kifo cha mchezaji wa kimataifa wa Cameroon Albert Ebosse. Uamuzi umechukuliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF katika kiakao chake kilichofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia. Kabylie ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini humo hivyo kuwapa nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani. Hatua hiyo ya CAF imekuja kufuatia Shirikisho la Soka la Algeria kuitaka Kabylie kucheza mechi zake za nmyumbani bila ya mashabiki katika uwanja huru msimu huu. Ebosse alifariki dunia hospitalini mwezi uliopita kutokana na majeraha ya kichwa yaliyosababishwa na kupigwa na kitu kizito na mashabiki wa klabu hiyo ambao walikasirishwa na kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa wapinzani wao USM Algers.
No comments:
Post a Comment