Tuesday, September 23, 2014

KOUYATE NJE WIKI SITA.

KIUNGO wa klabu ya West Ham United, Cheikhou Kouyate atakaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita baada ya kupata majeruhi ya nyonga. Kouyate aliumia wakati wa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Liverpool ambapo walishinda ka mabao 3-1. Kiungo huyo huenda akakosa michezo mitano ya ligi kuu ya England iliyo mbele yao ukiwemo ule wa dhidi ya Manchester United utakaopigwa Septemba 27 mwaka huu. Kouyate alihamia West Ham akitokea Anderlect kwa kitita cha paundi milioni saba Julai na toka ametua hapo ameonyesha kiwango cha hali ya juu.

No comments:

Post a Comment