Tuesday, September 23, 2014

HUWEZI KUMFANANISHA GOTZE NA RIBERY - BECKERNBAUER.

RAIS wa heshima wa klabu ya Bayern Munich, Franz Beckenbauer amesisitiza kuwa Mario Gotze hawezi kufananishwa na Franck Ribery kwakuwa ni wachezaji wa aina ya tofauti. Nyota huyo wa zamani wa Borussia Dortmund alihamishwa nafasi yake na kocha Pep Guardiola kutoka kati kwenda wingi ya pembeni mara kadhaa wakati Ribery alipokuwa kijiuguza. Hata hivyo, Beckernbauer haoni kama Gotze ni mchezaji muafaka kuziba nafasi ya Ribery. Nguli huyo wa soka wa zamani amesema huwezi kumuiga mtu kama Ribery kutokana na aina yake ya uchezaji ya kutanua uwanjani ili kuwavuta mabeki wa upinzani. Beckernbauer aliendelea kudai kuwa Gotze yuko tofauti na anadhani anafaa kwa mbinu za Guardiola kwani anapenda kucheza kitimu zaidi kwa kutoa pasi za haraka ila inabidi aongeze bidii kukuza kiwango chake. Gotze mwenye umri wa miaka 22 amefunga mabao mawili katika mechi saba za mashindano yote alizocheza za Bayern msimu huu.

No comments:

Post a Comment