Monday, September 22, 2014

TAJIRI WA PSG AMPA UHAKIKA BLANC PAMOJA NA MATOKEO MABOVU.

RAIS wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG Nasser Al-Khelaifi amemuhakikishia meneja wa klabu hiyo kuwa kibarua chake hakipo hatarini pamoja na kuanza vibaya msimu wa ligi. PSG iling’ang’aniwa sare ya bao 1-1 nyumbani na Olympique Lyon mwishoni mwa wiki hii na kwasasa wanashika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu wakiwa wameshinda mechi mbili pekee kati ya sita walizocheza. Huku pia wakiwa wametoa sare katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ylaya dhidi ya Ajax Amsterdan, tetesi juu ya kibarua cha Blanc zikavuma kwa kasi lakini Al-Khelaifi amezima tetesi hizo kwa kusisitiza kuwa kocha huyo ataendelea kuinoa PSG mpaka mwishoni mwa msimu. Akihojiwa Al-Khelaifi amesema pamoja na kiwango kisichoridhisha walichoanza nacho lakini ana uhakika watafanya vizuri katika siku za mbele na kuonyesha imani kwa Blanc. Blanc mwenye amesema anajua siku zote matokeo mabaya lazima yalete mkanganyiko lakini ana matumani hali hiyo itakwisha baada ya kurejesha makali yao na kuanza kushinda mechi zao.

No comments:

Post a Comment