Monday, September 22, 2014

VITA YAPIGA HATUA MOJA KUELEKEA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA.

KLABU ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC jana ilifanikiwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika. Mabao ya Vita katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Tata Raphael jijini Kinshasa yalitupiwa kimiani na Firmin Ndombe Mubele na Heritier Luvumbu Nzinga huku lile la kufutia machozi la Sfaxien likifungwa na Ali Maaloul. Vita watakwenda katika mchezo wao wa marudiano wiki ijayo wakijua sare ya aina yoyote inaweza kuwapeleka fainali ambapo watakutakana na aidha Etente Setif ya Algeria au TP Mazembe ya DRC. Sfaxien ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho na Super Cup walionekana kuzimiliki vyema dakika 20 za mwisho katika mchezo huo lakini walishindwa kutafuta nafasi ya kusawazisha. Sasa timu hizo zinatarajiwa kukutana katika mchezo wa marudiano Sepetmba 27 ili kuamua atayekwenda fainali inayotarajiwa kuchezwa kwa mikondo miwili kati ya Octoba 25-26 na Novemba 1-2.

No comments:

Post a Comment