RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter amethiboitisha kuwa atatetea kiti chake hicho katika uchaguzi ujao wa shirikisho hilo. Akihojiwa jijini Manchester Blatter mwenye umri wa miaka 78 alithibitisha uamuzi wake huo kuhu akidai atatoa taarifa rasmi katika mkutano mkuu wa kamati ya utendaji ya FIFA utakaofanyika Septemba 25 na 26. Tayari rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA Michel Platini ameshatangaza kutogombea nafasi hiyo ya Blatter. Blatter ambaye amekuwa katika kiti hicho cha FIFA toka mwaka 1998 amesema amechukua uamuzi huo kwasababu kazi alioianza anaona bado haijamalizika.
No comments:
Post a Comment