Monday, September 8, 2014

PAMOJA USHINDI, LOW AONYESHA KUTORIDHISHWA NA KIWANGO CHA UJERUMANI.

KOCHA wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low ameonyesha kutoridhishwa na matokeo ya ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya mwakani dhidi ya Scotland jana, lakini amefurahi kupata alama zote tatu muhimu. Kikosi cha Ujerumani kilionekana kucheza chini ya kiwango katika mchezo huo uliochezwa huko Dortmund lakini mabao mawili yaliyofungwa na Thomas Muller yalitosha kuwahakikishia ushindi. Katika mchezo huo Muller ndio aliyewapa wenyeji bao la kuongoza katika dakika 18 lakini bao hilo lilisawazishwa kupitia kwa Ikechi Anya katikati ya kipindi cha pili na kuepelekea wasiwasi kwa Ujerumani kabla Muller kufunga bao lingine dakika za mwishoni. Akihojiwa Low amesema makosa machache yaliyofanywa na baadhi ya wachezaji yalitaka kuwagharimu katika mchezo huo lakini anashukuru kwamba wamefanikiwa kuondoka na alama zote tatu. Low aliendela kudai kuwa ni jambo la muhimu kuanza na ushindi na alitegemea kuwa mchezo huo utakuwa mgumu.

No comments:

Post a Comment