WAKALA wa kocha Rafael Benitez amedai kuwa mteja wake huyo ameshakataa mara mbili nafasi ya kuinoa klabu ya Real Madrid wakati akiwa Liverpool. Benitez alikaa Anfield kwa misimu sita akiisaidia Liverpool kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Super Cup, Kombe la FA na Ngao ya Jamii. Mafanikio aliyopata Benitez akiwa Liverpool ndio yaliyochochea kuwindwa na vilabu mbalimbali ikiwemo Madrid kama anavyosema wakala wake Manuel Garcia Quilon. Wakala huyo amesema Benitez alipokea ofa hiyo kutoka kwa Madrid miaka mitano iliyopita na mwaka mwingine kabla. Quilon aliendelea kudai kuwa ili kumshawishi aweze kukubali ofa hiyo rais wa Madrid Florentino Perez alisafiri mwenyewe kwa ndege binafsi kwenda Uingereza kujaribu kumshawishi mke wa Benitez lakini hakufanikiwa. Benitez pia amewahi kuzinoa timu za Chelsea na Inter Milan kabla ya kujiunga na Napoli mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment